Kocha Cheche ataja kikosi cha wanandinga 23 kufuzu Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Kocha wa timu ya taifa ya wanawake walio chini ya umri Wa miaka 17 Mildred Cheche, ametaja kikosi cha wanandinga 23 kitakachochuana na Namibia katika raundi ya kwanza kufuzu Kombe la Dunia wiki ijayo.

Timu hiyo maarufu kama Junior Starlets itazuru Namibia kumenyana na wenyeji Ijumaa ijayo kabla kuandaa mkomdo wa pili jijini Nairobi April 17.

Kocha Cheche amewajumusha wengi Wa wachezaji walioshiriki mechi za awali za kufuzu mwaka jana.

Baadhi ya wachezaji walioitwa kikosini ni Lindey Weey, Brenda Awuor, Mwanakombo Bakari, Grace Mumo, Faith Boke, Brenda Achieng, na Fleviah Khatenje ambao wote walikuwa kikosini awali.

Mechi za raundi ya pili zitapigwa mwezi ujao huku raundi ya tatu ilisakatwa Julia.

Share This Article