Naibu Rais Kithure Kindiki ameelani vurumai zilizotokea katika mkutano wa chama cha UDA, aliokuwa akiongoza Jumamosi katika uwanja wa Nembure,kaunti ya Embu,akitaka wahuni waliohusika kukabiliwa kisheria.
Kundi la vijana wahuni lilivamia mkutano huo kuteketeza magari na kuharibu mali na kuwalazimu waliokuwa wakihudhuria mkutano huo akiwemp Kindiki kukimbilia usalama.
Mkutano huo ulikuwa umepangwa na Gavana wa Embu Cecily Mbarire.
Polisi walilazimika kurusha vitoza machozi ili kuwatawanya wahuni hao waliokuwa wakivamia mkutano huo.
Yakimi watu kadhaa walijeruhiwa katika mshikemshike huo.