Shirikisho la ngumi nchini Kenya BFK limetaja orodha ya mabondia is 40 ,watakaoshiriki mashindano ya ndondi barani Afrika jijini nairobi kati ya Oktoba 12 na 28 mwaka huu.
Wanamasumbwi hao tayari wako mazoezini katika eneo la Mathare Police Depot ,kabla ya kikosi cha mwisho kutajwa.
Kikosi hicho kinajumuisha mabondia chipukizi na walio na tajriba.
Zaidi ya mataifa 20 yanatarajiwa kushiriki mashindano hayo yatakayoleta pamoja mabondia bora barani Afrika.
Mashindano hayo yataandaliwa katika ukumbi wa Kasarani.