Kenya imejiunga rasmi na benki ya uwekezaji na ustawishaji miundombinu ya Asia (AIIB), baada ya kulipa ada zote zinazohitajika kujiunga na benki hiyo.
Hayo yalitangazwa leo Jumanne na Rais William Ruto, alipozuru makao makuu ya benki hiyo Jijini Beijing Uchina, ambapo Kenya ilitia saini ya makubaliano.
Kenya sasa ni miongoni mwa nchi 13 ambazo zimejiunga rasmi na benki hiyo, huku ikilenga kunufaika na benki hiyo kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo.
“Uanachama huo utaiwezesha Kenya kupata ufadhili kwa miradi ya miundo mbinu, juhudi za kukabiliana na tabia nchi, uunganishwaji, ushirikiano wa kikanda na teknolojia,” alisema Rais Ruto.
Benki hiyo inalenga kufadhili asilimia 50 ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kufikia mwaka 2025.
Rais Ruto anahudhuria kongomano la ushirikiano kati ya Uchina na Afrika (FOCAC),Jijini Uchina.