Balozi wa Azerbaijan nchini Kenya Sultan Hajiyev amesema nchi yake itatoa msaada wa pesa na utaalam kuelekea kwa Kongamano la pili la Miji barani Afrika mwezi ujao.
Aidha, aliongeza kuwa Azerbaijan itatumia kongano la Kenya kujiandaa kwa Kongamano la Miji Duniani, litakaloandaliwa nchini Azerbaijan mwezi Mei mwaka huu.
Akizungumza punde baada ya kusaini mwafaka wa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, Waziri wa Ardhi Alice Wahome alikariri kuwa serikali iko tayari kuandaa kongamano la kufana.
Aliongeza kuwa itakuwa fursa bora kwa Kenya kudhihirishia bara ufanisi wake katika ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.
Kongamano hilo la pili litaandaliwa kati ya tarehe 8 na 10 mwezi ujao.