Timu ya taifa ya kenya ya mpira wa wavu kwa wanawake Malkia Strikers, itachuana na Algeria katika robo fainali ya mashindano ya Afrika kwa wanawake.
Wenyeji Kenya walifuzu kwa kwota fainali kufuatia ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Nigeria, katika raundi ya 16 bora siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Kasarani.
Kenya walitawala pambano hilo kwa seti za 25-21,25-17 na 25-15.
Cameroon watakumbana na Uganda katika mechi nyingine yar obo fainali huku mshindi akiweka miadi na mshindi baina ya Kenya na Algeria kwenye nusu fainali.