Junior Starlets wapiga mazoezi ya mwisho kabla ya kuchuana na Namibia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka kwa wanawake wasiozidi umri wa miaka 17 imefanya mazoezi ya mwisho siku ya Jumamosi mjini Windhoek ,Namibia kabla ya pambano la Jumapili kufuzu kwa Kombe la dunia dhidi ya wenyeji.

Kenya chini ya ukufunzi wa kocha Mildred Cheche inawania kufuzu kwa kombe la dunia litakaloandaliwa nchini Morocco mwaka huu kwa mara ya pili.

Junior Starlets walijikatia tiketi kwa kombe la dunia miaka miwili iliyopita katika Jamhuri ya Domonika.

Kenya wataanda mchuano wa marudio wiki ijayo jijini Nairobi.

Share This Article