Israel imesahmbulia na kuwaua watu 14 Kusini mwa mji mkuu wa Lebanon,Beirut siku ya Jumapili, siku moja baada ya kutishia kutekeleza shambulizi hatua iliyolazimu Syria kufunga mpaka wake na Lebanon.
Shambulizi hilo la mapema Jumapili na majeshi ya Israel lilisababisha kuawa kwa watu wanne na wengine sita wa familia moja.
Watu wengine 39 walijeruhiwa katika mji wa Jnah ulio karibu na Beurut, kulingana na Wizara ya afya ya umma nchini Lebanon.
Haya yanajiri huku pia Marekani ikitoa onyo la kutekeleza mashambulizi mapya nchini Iran ,hali ambayo imeifanya iran kuitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati.