Idadi ya walioangamia kwa mafuriko nchini Kenya yafikia 110

Dismas Otuke
1 Min Read

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoshuhudiwa  katika maeneo mbalimbali nchini imefikia 110.

Aidha, idadi ya kaunti zilizoathiriwa na mkasa huo imefikia 30, kulingana na takwimu za hivi punde kutoka kwa Wizara ya Usalama wa Kitaifa.

Kaunti zingine zilizokumbwa na mafuriko ni Kilifi, Bungoma, Kiambu, Uasin Gishu, Nyeri, Kirinyaga, Nyandarua na Mandera.

Kaunti ya Nairobi imenakili visa vingi ikiwa na watu 37 waliofariki, ikifuatwa na eneo la Mashariki likiwa na vifo 26.

Watu 14 wameangamia katika Bonde la Ufa, huku  Nyanza ikiwa na 11, na maeneo ya Kati na Pwani yakiwa na idadi ya vifo sita na vitano mtawalia.

Eneo la Magharibi limesajili vifo viwili.

Takriban watu 34,000 wameachwa bila makao baada ya nyumba zao kusombwa au kujaa maji ya mafuriko.

Share This Article