Serikali ya kaunti ya Homa Bay imezindua chanjo ya Lenacapavir, hatua inayolenga kuzuia msambao wa virusi vya HIV/AIDS katika kaunti hiyo.
Uzinduzi huo ulitekelezwa katika hospitali ya level 4 ya Kendu Bay Level 4 na Gavana wa kaunti hiyo Gladys Wanga.
Hatua inatarajiwa kuzuia maambukizi ya virusi kwa HIV ambavyo ni vya kiwango cha juu katika kaunti hiyo
Kwenye uzinduzi huo, Gavana Wanga alisema kuanzishwa kwa chanjo hiyo, kunaleta matumaini ya kupungua kwa maambukizi mapya hususan miongoni mwa vijana.
Huku takriban watu Milioni 1.4 wakiishi na virusi vya HIV na maelfu ya maambukizi mapya yakinakiliwa kila mwaka, juhudi za kuzuia maambukizi mapya ndiyo mkakati bora dhidi ya vita hivyo.