Wizara ya Fedha imo mbioni kutafuta pesa za kuendelesha mpango wake wa kudhibiti bei ya mafuta katika masoko ya humu nchini.
Kulingana na Waziri John Mbadi, serikali inatafuta hela zaidi ili kuhakikisha mpango huo unaendelea hadi wakati wa uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Serikali ilianzisha mpango huo kufuatia mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati na kuathiri bei ya mafuta katika vituo vya kuuza mafuta nchini.
Hata hivyo, Mbadi hajataja mbinu serikali itatumia kutafuta hela hizo, akiongeza kuwa huenda bei ya mafuta ikashuka zaidi na kuwapunguzia wananchi bei punde wasambazaji watakapolipwa pesa hizo.