Waziri wa Fedha na Mipango ya Taifa John Mbadi ameitengea sekta ya viwanda shilingi bilioni 16.7, ili kupiga jeki utengenezaji bidhaa hapa nchini.
Akiwasilisha bejeti ya mwaka 2026/2027 kwenye Majengo ya Bunge siku ya Alhamisi, Waziri huyo alisema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 2.6 zitatumika katika maeneo ya kiviwanda ya kauti, shilingi billion 5.4 katika mradi wa upatikanaji wa fedha na kuimarisha biashara.
Wakati huo huo, shilingi bilioni 602 zimetengwa kwa maendeleo ya kampuni ya nguo ya Athi River, shilingi milioni 300 kwa uzinduzi wa kituo cha kushughulikia bidhaa za kuuza nje ya nchi, shilingi milioni 604 zitumike kwa uzinduzi wa maeneo ya kiuchumi ya Naivasha na shilingi bilioni 2.4 zikitengwa kwa mageuzi ya kiuchumi na ajira hapa nchini.
Waziri huyo alidokeza kuwa hatua hizo zimechukuliwa kuimarisha viwanda vya hapa nchini na kubuni nafasi za ajira za ubora wa hali ya juu.