Guterres ana wasiwasi baada ya mapigano kuzuka tena kati ya Marekani na Iran

radiotaifa
1 Min Read
Antonio Guterrs - Katibu Mkuu wa UN / Picha kwa hisani ya AFP

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezitaka Marekani na Iran kusitisha mapigano na kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

“Katibu Mkuu amekuwa na wasiwasi kwa muda sasa kwamba pande hizo mbili zisiporeje kwenye meza ya mazungumzo, wigo wa mzozo unaweza kupanuka, na inaonekana ndivyo hali ilivyo katika saa za hivi karibuni,” Farhan Haq aliwaambia waandishi wa habari mjini New York.

Kwa mujibu wake: “Kinachoendelea sio kitu kizuri – Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa – anataka pande hizo kusitisha mapigano na kurejea tena kwenye juhudi za kidiplomasia.”

Msemaji huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliongeza kusema: “Juhudi za upatanishi zinazofanywa na Pakistan, Qatar na nchi nyingine zinaendelea.”

Taarifa ya BBC

Share This Article