Chama cha soka nchini Ghana kinadaiwa kuzungumza na kocha kutoka Ufaransa Hervé Renard, ili kutwaa ukufunzi wa timu ya taifa Black Stars kuanzia kwa fainali za Kombe la Dunia mwezi Juni mwaka huu.
Baadhi ya vipengee muhimu vilivyo kwenye meza ya mazungumzo ni kiwango cha makataba huo,wasaidizi wake na masharti mengine, kabla ya uamuzi wa mwisho kuafikiwa baina ya pande zote mbili.
Renard mwenye umri wa miaka 57, amekuwa mkufunzi mkuu wa timu ya Saudi Arabia tangu mwaka 2024, na alikuwa afurushwe wakati wowote kufuatia msururu wa matokeo duni kwenye maandalizi ya kuelekea Kombe la Dunia.
Ghana ilimpiga kalamu kocha mkuu Otto Addo, mepema wiki hii zikiwa takriban siku 70, kabla ya kuanza kwa dimba la Kombe la Dunia kutokana na matokeo mabovu.
Black Stars wamejumuishwa kundi L katika kipute cha Kombe la Dunia pamoja na Uingereza,Croatia na Panama.