Garby Thomas na Wanyonyi kushiriki Kip Keino Classic

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Olimpiki Garby Thomas wa Marekani na Emmanuel Wanyonyi wa Kenya ndio wa hivi punde kuthibitisha kushiriki makala ya saba ya mashindano ya Kip Keino Classic continental Tour, yatakayoandaliwa katika uwanja wa Nyayo tarehe 24 mwezi huu.

Thomas aliye na umri wa miaka 29 na aliyeshinda dhahabu ya Olimpiki mwaka 2024 jijini Paris atatimka mita 100 huku Wanyonyi aliyenyakua dhahabu ya mita 800 akishiriki mbio za mita 1500.

Mashindano ya mwaka huu ambayo yataandaliwa majaira ya jioni yamewavutia wanariadha maahiri wa kutoka humu nchini na wale wa kimataifa.

Kama njia ya kuhakikisha wanariadha wanakiambia muda wa kasi mfumo wa teknolojia ya Wave lighgt  utatumika kwa mara ya kwanza.

 

Share This Article