EPRA yapunguza bei ya diesel kwa shilingi 5

Kufuatia mabadiliko hayo, Jijini Nairobi lita moja ya petroli itauzwa shilingi 214.03, diesel shilingi 217.86 na mafuta taa shilingi 191.38.

Tom Mathinji
1 Min Read
EPRA yapunguza bei ya diesel, bei ya Petroli na Mafuta Taa zakosa kubadilika.

Halmashauri ya kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA) imepunguza bei ya mafuta ya diesel kwa shilingi tano, huku bei za petroli na mafuta taa zikikosa kubadilika.

Kwenye taarifa iliyotolewa na halmashauri hiyo leo Ijumaa, bei hizo mpya zitatumika kati ya Agosti 15 na Septemba 14.

“Bei ya mafuta ya diesel imepungua kwa shilingi tano, huku bei za petroli na mafuta taa zikisalia zilivyo kutokana na mikakati ya udhibiti ya serikali ya shilingi milioni 938,” ilisema EPRA kwenye taarifa.

Kufuatia mabadiliko hayo, Jijini Nairobi lita moja ya petroli itauzwa shilingi 214.03, diesel shilingi 217.86 na mafuta taa shilingi 191.38.

Halmashauri hiyo hufanyia mabadiliko bei za mafuta kila mwezi, kuambatana na mabadiliko ya bei za kimataifa, ushuru na ruzuku za serikali, kabla ya kuweka bei za rejareja zitakazotumika kote nchini.

TAGGED:
Share This Article