EPRA yadumisha bei ya mafuta

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka ya kudhibiti kawi na bidhaa za petrol nchini (EPRA), imetangaza kuwa bei ya mafuta itasalia ilivyokuwa katika kipindi cha mwezi mmoja ujao kati ya Machi 15 na Aprili 15 mwaka huu.

Kulingana na tangazo hilo, mafuta ya petroli yatauzwa kwa shilingi 178.28, kwa kila lita moja katika kaunti ya Nairobi, wakati dizeli ikiuzwa kwa shilingi 166.54, nayo mafuta ya taa yatauzwa kwa shilingi 152.78, kwa mwezi mmoja ujao.

Hatua hii inaondoa mbali hofu iliyokuwa imetanda kuhusu uwezekano wa kuwa na upungufu wa mafuta nchini, hali ambayo ingechangia kuongezeka kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu.

Hii ni kutonana na mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, hali ambayo imeathiri vibaya eneo la ghuna ambalo huzalisha mafuta mengi.

TAGGED:
Share This Article