DCI wachunguza kushambuliwa kwa Seneta Osotsi

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa ujasusi wamelaani vikali kushambuliwa kwa  Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi,  hapo jana katika mkahawa Java  katika jumaba la West End Mall, kaunti ya  Kisumu.

DCI imesikistishwa na kitendo hicho cha kinyama ikiongeza kuwa inafanya uchunguzi kwa usaidizi wa video za CCTV za jumba hilo.

Hata hivyo Polisi wametaka umma kukoma kueneza uvumi  na kupisha uchunguzi kufanyika  .

Aidha, DCI imekariri kujitolea kupata chimbuko la shambulizi hilo  na kuwakamata na kuwaadhibu kisheria wote waliohusika.

Osotsi alishambuliwa na kujeruhiwa na kundi la vijana ambao hawajatambulika na kujeruhiwa jana na yuko hospitalini akipokea matibabu.

Share This Article