Klabu ya Chelsea ilijikatia tiketi kwa fainali ya klabu bingwa duniani baada ya kuwabandua Fluminense kutoka Brazil, mabao 2-0, kwenye nusu fainali iliyosakatwa jana Jumanne usiku katika uwanja wa Metlife mjini New Jersey.
Joao Pedro alipachika mabao yote, moja katika kila kipindi, na kuwapa The Blues ushindi maridhawa.
Nusu fainali ya pili itakasatwa leo usiku baina ya mabingwa wa Ulaya Paris St Germain, PSG kutoka Ufaransa dhidi ya Mabingwa mara 15 wa Ulaya Real Madrid.
Fainali ya kipute hicho itasakatwa Jumapili hii, Julai 13 katika uchanjaa wa Metlife.