Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limefungua rasmi Makao Makuu ya uratibu wa michuano ya AFCON 2027, Jijini Dar es Salaam Tanzania.
Ufunguzi huo unaashiria hatua zilizopigwa kwa maandalizi ya pamoja kati ya Kenya, Tanzania na Uganda, kuandaa mashindano hayo, kupitia ushirikiano wa kikanda, kitaasisi na uwajibikaji wa pamoja.
Makao Makuu hayo yamejukumiwa kuratibu, kutoa mipango, na kuendesha michuano hiyo inayofanyika kati ya Juni 19 na Julai 17, 2027, ikisimamiwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya, na Uganda
Wakati huo huo Kenya na Uganda zitaendelea kuwa na afisi za kiutendaji katika miji mikuu yao, ili kusaidia uratibu wa pamoja
CAF imeipongeza Kenya kwa hatua ilizopiga kwa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Raila Odinga, uwanja wa michezo wa Kasarani na viwanja vingine 12 vitakavyotumika kwa mazoezi.