Bunge la Taifa laidhinisha matumizi ya fedha za umma 2026/2027

Hatua hiyo inaashiria kuwa bunge hilo limekubali kiwango cha matumizi ya serikali kuu na kiwango ambacho kila sekta itapokea kabla ya kutayarishwa kwa makadirio ya bajeti.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kikao cha Bunge la Taifa.

Bunge la Taifa limeidhinisha matumizi ya fedha za umma ya mwaka wa fedha 2026/2027, huku bajeti ya taifa ikiwa shilingi trilioni 2.878.

Hatua hiyo inaashiria kuwa bunge hilo limekubali kiwango cha matumizi ya serikali kuu na kiwango ambacho kila sekta itapokea kabla ya kutayarishwa kwa makadirio ya bajeti.

Kati ya kiwango hicho, serikali kuu imetengewa shilingi trilioni 2.797, bunge shilingi bilioni 50.78 huku idara ya mahakama ikitengewa shilingi bilioni 30.44.

Serikali za kaunti zimetengewa shilingi bilioni 420, hii ikiwa ni nyongeza ya shilingi bilioni 5 ikilinganishwa na mgao wa mwaka jana.

Kwenye mgao huo katika sekta ya elimu, shilingi bilioni 160 zimetengewa vyuo vikuu na utafiti, huku shilingi bilioni 134.7 zikitengewa elimu ya msingi.

Katika sekta ya usalama, Huduma ya Taifa ya Polisi itapokea shilingi bilioni 143.2 huku Wizara ya Ulinzi ikipokea shilingi bilioni 241.

Maendeleo ya Miundombinu pia yamepewa kipaumbele, ambapo idara ya barabara imepokea mgao wa shilingi bilioni 232, huku sekta ya nyumba ikipata shilingi bilioni 139.

Share This Article