Bolsonaro alazwa hospitalini

Amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi hospitalini kutokana na maradhi ya homa ya mapafu

Marion Bosire
1 Min Read
Aliyekuwa Rais wa Brazil Jair Bolsonaro.

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, aliyefungwa jela kwa kupanga mapinduzi baada ya kushindwa kwenye uchaguzi amelazwa hospitalini.

Bolsonaro amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi hospitalini kutokana na maradhi ya homa ya mapafu.

Hospitali ya DF Star jijini Brasilia ilitoa taarifa jana Jumamosi ikisema kwamba kiongozi huyo wa zamani wa umri wa miaka 70 yuko imara.

Hata hivyo taarifa hiyo ilielezea kwamba anakumbwa pia na matatizo ya figo na kutokana na hilo, haijulikani ataondoka lini hospitalini.

Bolsonaro alikuwa rais wa Brazil mwaka 2019 hadi 2023 na alilazwa hospitalini Ijumaa akiwa na joto jingi mwilini, ueneaji duni wa oksijeni, kutokwa jasho na kuhisi kibaridi.

Anatumikia kifungo cha miaka 27 gerezani adhabu aliyopatiwa kutokana na makosa ya kupanga mapinduzi na hii sio mara ya kwanza anakumbwa na matatizo ya mfumo wa kupumua.

Mwaka 2018 alidungwa kisu tumboni akiwa kwenye mkutano wa siasa na tangu wakati huo amekuwa akikumbwa na matatizo ya kiafya.

Share This Article