Bobi Wine atangaza kutoroka Uganda

Dismas Otuke
1 Min Read

Aliyekuwa Mwaniaji Urais nchini Uganda Robert Kyakulanyi, maarufu kama Bobi Wine ametangaza kutorokea uhamishoni kwa kuhofia kudhulumiwa na serikali ya Rais Yoweri Museveni.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu aende mafichoni, Wine amesema kuwa maafisa wa polisi wamekuwa wakifanya msako nyumbani kwake na kwa wandani wake bila mafanikio.

Aidha Wine amemkemea Rais Museveni, kwa kile alichokitaja kuwa wizi wa wazi katika uchaguzi mkuu uliopita mapema mwaka huu akiahidi kuendeleza kampeini nje ya nchini za kuwakomboa Waganda.

Museveni alingazwa mshindi wa uchaguzi wa Januari mwaka huu alipozoa kura milioni 7.9 dhidi ya milioni 2.7 za Wine.

 

Share This Article