Biwi la simanzi latanda Homa Bay ,mwili wa Were ukiwasilishwa

Haya yanajiri huku idara ya ujasusi ikifichua kuwa imewakamata washukiwa wakuu katika mauaji hayo .

Dismas Otuke
1 Min Read

Biwi la simanzi limetanda leo katika kaunti ya Homa Bay, wakati mwili wa mbunge wa eneo la Kasipul Charles Ong’ondo Were, ulipowasilishwa kwa mazishi mapema leo.

Msafara mkubwa wa magari umeonekana ukisindikiza gari lililobeba mwili wa marehemu mbunge huyo kutoka uwanja wa mdogo wa ndege wa Kapunde, ukiongozwa na Gavana Gladys Wanga, na mbunge wa Homa Bay mjini Peter Kaluma.

Marehemu Were aliyefariki baada ya kupigwa risasi wiki jana na mtu asiyejulikana katika barabara ya Ngong jijini Nairobi atazikwa kesho Ijumaa, nyumbani kwake katika kijiji cha Kachien eneo bunge la Kasipul.

Misa ya wafu kwa marehemu iliandaliwa jana katika kaunti ya Nairobi kabla ya mwili kusafirishwa kutoka uwanja wa ndege wa Wilson mapema leo.

Haya yanajiri huku idara ya ujasusi ikifichua kuwa imewakamata washukiwa wakuu katika mauaji hayo .

Website |  + posts
Share This Article