Barca yamsajili Rodri kwa kima cha pauni milioni 51 hadi mwaka 2030

Nahodha huyo wa Uhispania anaongeza makali katika kiungo cha kati cha Barca, ambacho tayari kinasheheni Pedri, Gavi, Frenkie de Jong, Marc Bernal, Dani Olmo na Fermín López.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Uhispania FC Barcelona, wamekamilisha usajili wa kiungo Rodri kutoka Manchester City, kwa kima cha pauni milioni 51 hadi mwaka 2030.

Rodri,aliye na umri wa miaka 30,amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kukataa ofa ya Real Madrid.

Nahodha huyo wa Uhispania anaongeza makali katika kiungo cha kati cha Barca, ambacho tayari kinasheheni Pedri, Gavi, Frenkie de Jong, Marc Bernal, Dani Olmo na Fermín López.

Rodri alitokea Villarreal na baadaye kutua Atlético Madrid, kabla ya kujiunga na Mancity mwaka 2019.

Kufikia leo ameshinda mataji manne ya Ligi Kuu Uingereza,moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya,taji ya Ulaya (Euro),UEFA Nations League na akiwa na Uhispania, kutajwa mchezaji bora wa Euro na UEFA Nations League pamoja na Ballon d’Or .

Share This Article