Awamu ya kwanza ya mazungumzo baina ya Marekani na Iran yamekamilika katika mji mkuu wa Islamabad nchini Pakistan.
Fununu zadokeza kuwa pande zote mbili zinashauriana kwa jumbe za maandishi na ni mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya Marekani na Irani tangu mwaka 1979.
Ujumbe wa mazunguzo wa Marekani unaongozwa na Makamu Rais JD Vance wakati uaonde wa Iran ukiwashirikisha Spika wa Bunge Mohammad Bagher Ghalibaf na waziri wa mambo ya kigeni Abbas Araghchihuku Waziri mkuu wa Pakistan akiwa mshirikishi wa mazungumzo hayo.
Haya yanajiri huku wizara ya afya nchini Lebanon ikitangaza Jumatano wiki hii kuwa idadi ya raia wake waliouawa na majeshi ya Israel imefikia 357.