Alliou Cisse asaini mkataba wa miaka minne kuifunza wa Angola

Dismas Otuke
1 Min Read

Aliyekuwa kocha na mchezaji wa Senegal Alliou Cisse, amejulishwa rasmi siku ya Alhamisi kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Angola kwa mkataba wa miaka minne.

Cisse aliye na umri wa miaka 50, amejukumiwa kuifuzisha Angola kwa fainali za AFCON mwaka 2027, pamoja na kubuni kikosi imara kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2030.

Cisse ambaye ni beki wa zamani alikuwa nahodha Teranga Lions, ilipofika hadi hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2002.

Aidha, aliwaongoza Senegal kunyakua Kombe la AFCON kwa mara ya kwanza mwaka 2021.

Hadi uteuzi wake Cisse amekuwa kocha wa tmu ya taifa ya Libya hadi alipogura maajuzi.

Share This Article