Mbunge wa zamani wa Tetu Francis Thombe Nyammo ameaga dunia.
Akitangaza kifo hicho, Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetangula, alimtaja marehemu Nyammo kuwa mtu atakayekumbukwa kwa uongozi wake wa kipekee na aliyejitolea kushughulikia maslahi ya umma.
“Atakumbukwa kwa utendakazi wake, uongozi na kujitolea kuhudumia jamii,” alisema Spika Wetangula.
“Natuma rambirambi kwa familia yake, marafiki na wakazi wa Tetu kwa jumla,” aliongeza spika huyo.
Nyammo ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 86.