Ajali ya Webuye: Ruto azifariji familia zilizoathirika

Kiongozi wa nchi amezitaka asasi husika kukabiliana na ukiukaji wote wa sheria za barabarani ili kuhakikisha usalama barabarani kote nchini. 

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais William Ruto

Rais William Ruto ametuma risala za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajali kwenye barabara ya Kitale-Webuye, kaunti ya Bungoma. 

Watu wasiopungua 15 walifariki kwenye ajali hiyo iliyotokea jana Jumatatu usiku huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Ajali hiyo inadaiwa kusababishwa na dereva wa lori la masafa marefu ambaye alipoteza mwelekeo na kugonga magari kadhaa pamoja na wapita njia.

“Rambirambi zetu ni kwa familia za waathiriwa wa ajali ya kutisha huko Webuye, kaunti ya Bungoma iliyotokea jana usiku,” alisema Rais Ruto kwenye risala yake.

“Mwenyezi Mungu na azipe nguvu familia zilizoathiriwa kustahimili msiba huu. Pia tunawatakia afueni ya haraka majeruhi.”

Kiongozi wa nchi amezitaka asasi husika kukabiliana na ukiukaji wote wa sheria za barabarani ili kuhakikisha usalama barabarani kote nchini.

Share This Article