Afueni kwa wakazi kufuatia kuzinduliwa kwa kituo cha matibabu Lodwar

radiotaifa
1 Min Read

Taarifa ya Philip Ekadeli

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Fred Hollows likishirikiana na serikali ya kaunti ya Turkana, limezinduwa kituo cha matibabu ya macho mjini Lodwar.

Wakizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye hospitali ya rufaa mjini Lodwar, afisa mkuu wa Fred Hollows, Ben Kolwa, amesema mradi huo unaogharimu millioni tisa unalenga kuhudumia mamia ya wagonjwa wa
macho, huku ukitarajia kukusanya ushuru wa shilingi elfu mia tatu kwa mwezi.

Hata hivyo, waziri wa Afya kwenye kaunti hiyo Joseph Epem, amesema wakazi wa eneo hilo sasa watapata huduma kwa urahisi, ikilinganishwa na siku zilizopita ambapo walilazimika kusafiri hadi mjini Eldoret.

 

Share This Article