Afrika Kusini imemteua Roelf Meyer, kuwa balozi wake nchini Marekani baada ya Ebrahim Rasool kufurushwa na Rais Donald Trump Machi, 2025.
Uteuzi huo wa Meyer unaashiria lengo la Pretoria la kuimarisha uhusiano wake na Washington baada ya sintofahamu iliyoshuhudiwa kati ya nchi hizo mbili.
Meyer, mwenye umri wa miaka 78, ni mpatanishi mkongwe ambaye pia aliwahi kuwa waziri katika serikali iliyoongozwa na chama cha Apartheid Nationalist Party.
Umaarufu wake ulijulikana katika miaka ya 90, wakati wa siku za mwisho za utawla wa upaguzi wa rangi ambapo chama cha Nationalist kilishiriki mazungumzo na kile cha African National Congress (ANC) kumaliza ubaguzi na utawala wa wazungu.
Mazungumzo hayo yalisababisha kuandaliwa kwa uchaguzi wa kwanza wa demokrasia mwaka 1994.
Akiwa mpatanishi mkuu, Ralph alifahamiana na Rais wa sasa wa taifa hilo Cyril Ramaphosa, ambaye wakati huyo alikuwa mpatanishi wa ANC.