Afrika Kusini yamteua Pitso Mosimane kuwa kocha mkuu wa Bafana Bafana hadi mwaka 2030

Mosimane aliye na umri w amiaka 62, amethiubitishwa na kujulishwa rasmi kutwaa wadhfa huo kutoka kwa Hugo Broos, aliyeiongoza Afrika Kusini katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Pitso Mosimane ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Afrika Kusini hadi baada ya Kombe la Dunia mwaka 2030 nchini Morocco,Uhispania na Ureno.

Mosimane aliye na umri w amiaka 62, amethiubitishwa na kujulishwa rasmi kutwaa wadhfa huo kutoka kwa Hugo Broos, aliyeiongoza Afrika Kusini katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Mosimane atakuwa na siku 23 pekee kabla ya Bafana kucheza mechi ya kwanza ya kufuzu kwa fainali za AFCON hatua ya makundi dhidi ya Guinea mjini Pretoria.

Mataifa mengine kundini D na Afrika Kusini katika hatua ya makundi ya kufuzu ni Kenya na Eritrea.

Kocha huyo anarejea kwa mara ya pili katika wadhfa huo baada ya kuwa usukani kwa miaka miwili kuanzia mwaka 2010.

Mosimane ana rekodi nzuri akishinda taji ya Ligi ya mabingwa Afrika mara moja na Mamelodi Sundowns kabla ya kushinda mataji mawili ya Ligi ya mabingwa akiwa na Al Ahly ya Misri.

Share This Article