Naibu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Phumzile Mlambo-Ngcuka amefariki

Habari kuhusu mahali na wakati wa kufariki kwake, hazikutolewa na serikali wala chama chake cha African National Congress.

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Phumzile Mlambo-Ngcuka amefariki akiwa na umri wa miaka 71.

Naibu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Phumzile Mlambo-Ngcuka, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 71.

Mlambo-Ngcuka, ambaye alikuwa mwanaharakati dhidi ya sera ya ubaguzi wa rangi, alikuwa Naibu Rais tangu mwaka  2005 hadi  2008.

Habari kuhusu mahali na wakati wa kufariki kwake, hazikutolewa na serikali wala chama chake cha African National Congress.

Mlambo-Ngcuka alikuwa sehemu ya bunge la kwanza la kidemokrasia la chama cha ANC, baada ya kukamilika kwa ubaguzi wa rangi na utawala wa wazungu mwaka  1994, wakati ambapo Nelson Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa kidemokrasia wa taifa hilo.

“Mama Phumzile alikuwa kiongozi shupavu wa chama chetu na aliyejitolea kuwahudumia watu. Aliweka historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu wadhifa wa Naibu Rais,” kilisema chama cha ANC.

Amemuacha mume na watoto watano.

Share This Article