Wawili wafariki,22 wajeruhiwa Marsabit kutokana na vita vya Ethiopia

Majeshi ya Kenya yameimarisha doria huku yakiharibu grenedi kadhaa zilizorushwa na roketi na kuanguka upande wa Kenya kutoka Ethiopia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Angaa watu wawili wamefariki na wengine 22 kujeruhiwa huku wengine 10,000 wakitoroka makwao katika kaunti ya Marsabit kutoka na vita vinavyoendelea nchini Ethiopia.

Inaaminika kuwa vita hivyo vimezagaa kutoka nchini jirani ya Ethiopia katika eneo la Tigray, vikihusisha majeshi ya Tigray , majeshi ya Eritrea pamoja na majeshi ya Ethiopia.

Kulingana na Gavana wa Marsabit Mohamud Ali zaidi ya raia 50,000 wa Ethiopia wameingia nchini Kenya wakijaribu kukimbilia usalama.

Wakazi wa Moyale nchini Kenya wamekumbwa na makali ya vita vya Ethiopia katika mpaka wa Oromia na Somalia.

Majeshi ya Kenya yameimarisha doria huku yakiharibu grenedi kadhaa zilizorushwa na roketi na kuanguka upande wa Kenya kutoka Ethiopia.

Share This Article