Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, amezindua rasmi kampeni yake ya kutafuta muhula wa pili.
Rais huyo ameahidi kukuza uchumi, kukabiliana na ukosefu wa usalama na kutatua upungufu wa makazi nchini humo.
Katika ahadi zake, Tinubu ameahidi kukuza uchumi wa asilimia kwa 6 kila mwaka ifikapo 2031, kuongeza maafisa 78,000 wa usalama na kujenga nyumba 200,000 za gharama nafuu.
Nigeria inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Januari 2027, huku Peter Obi na aliyekuwa Makamu wa Rais Atiku Abubakar wakiwa miongoni mwa wapinzani wakuu wa Tinubu.
Tinubu alichaguliwa mwaka 2023 na kuanzisha mfululizo wa mageuzi ya kiuchumi, yakiwemo kuondoa ruzuku ya mafuta.
Taarifa ya BBC