Rais wa Cameroon Paul Biya, ametangaza kuywa uchaguzi wa ubunge na serikali za mitaa, utaandaliwa Februari 7, 20207, baada ya kuahirishwa mara mbili.
Biya, mwenye umri wa miaka 93, aliyasema hayo kupitia tangazo rasmi kwenye redio ya taifa siku ya Jumatatu.
Tangazo hilo la Biya, limejiri wakati ambapo Cameroon inakumbwa na hali taharuki huku utawala wa taifa hilo ukitekeleza misako kwa viongozi wa upinzani, mwaka mmoja baada ya Biya kushinda uchaguzi uliomuongezea muhula mwingine uongozini.
Biya, ambaye ameongoza Cameroon tangu mwaka 1982, ndiye Rais mkongwe zaidi duniani.
Kuchaguliwa kwake mwezo Oktoba mwaka jana, kulisababisha maandamano kote nchini humo, na kusaabisha utawala nchini humo kutekeleza msako mkali.
Serikali ya Biya imeahirisha uchaguzi wa ubunge na wa serikali za mitaa mara mbili, na kusababisha kuongezwa muhula wa wabunge hadi Disemba 20, 2026, huku muhula wa serikali za mitaa ukiongezwa hadi Februari 28, 2027.