Tiketi za mchuano wa kimataifa wa kirafiki baina ya miamba wa Ulaya Bayern Munich na Ajax Amsterderm kutoka Uholanzi katika uwanja wa Raila Odinga Januari 5,mwaka ujao zimeanza kuuzwa Alhamisi jioni.
Waziri wa Michezo Salim Mvurya amesema tiketi hizo zitauzwa kwa awamu kadhaa kupitia tovuti ya www.TalantaSportsCity.com.kati ya shilingi 2,500 na shilingi 20,000.
Aidha, Mvurya amefafanua kuwa ufadhili wa mechi hiyo ambayo itakuwa ya kufungua uchanjaa huo unaoselehi mashabiki 60,000, unafanywa na sekta ya kibinafsi na wala hamna hela zozote za umma zitakazotumika.
Pia waziri ameweka bayana kuwa timu zote mbili zimethibitisha kutuma vikosi vya kwanza huku pia Kenya ikiwa tayari kuandaa fainali za kufana za AFCON.
Pambano hilo litatumika kufungua rasmi uwanja wa Raila Odinga ambao utaandaa mechi za AFCON mwaka ujao pamoja na Tanzania na Uganda.
Munich wanajivunia kushinda taji ya ligi ya mabingwa Ulaya mara sita huku Ajax wakitawazwa mabingwa mara nne.