Majaribio ya chanjo mpya za Ebola kuanza DRC

Majaribio hayo ya chanjo mbili mpya yatafanywa na Shirika la Afya Duniani, WHO huku matokeo yakitarajiwa mapema mwakani.

Martin Mwanje
1 Min Read
Nigeria yathibitisha kisa cha kwanza cha Ebola.

Majaribio ya matibabu ya chanjo mbili zilizotengenezwa kwa ajili ya virusi aina ya Bundibugyo vinavyosababisha ugonjwa wa Ebola yanatarajiwa kuanza katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, DRC.

Majaribio hayo yatafanywa na Shirika la Afya Duniani, WHO.

Watu zaidi ya 10,000 wameambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini DRC.

Likitangaza mpango wa kuanza majaribio hayo jana Jumatano, WHO ilisema majaribio hayo yatafanywa chini ya idhini ya serikali ya DRC.

Matokeo yanatarajiwa kutolewa mapema mwakani.

Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ni Mkurugenzi Mkuu wa WHO. Anaonya kuwa  chanjo pekee haziweza zikakomesha mlipuko wa Ebola, lakini zinaweza zikawa zana mpya yenye nguvu ya kuudhibiti.

Idadi ya visa vya Ebola imekuwa ikiongezeka kwa kasi nchini DRC tangu mwezi Machi mwaka huu huku watu zaidi ya 5,000 wakiripotiwa kufariki kufikia Novemba Mosi, kwa mujibu wa WHO.

Share This Article