Naibu Rais Kithure Kindiki amewasili nchini Antigua and Barbuda, kuhudhuria mkutano wa 28 wa Jumuiya ya Madola kwa niaba ya Rais William Ruto.
Mkutano huo wenye kauli mbiu ” Kuchochea ushirikiano na uwekezakaji kwa ustawi wa Jumuiya ya Madola”, ulianda Novemba 1 na utakamilika Novemba 4, 2026.
Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Gaston Browne, atakuwa mwenyeji wa viongozi wa serikali watakaohudhuria mkutano huo, huku aliyekuwa gwiji wa mchezo wa kriketi Sir Vivian Richards akiteuliwa kuwa Mjumbe Maalum wa mkutano huo.
Kwenye mkutano huo, viongozi hao wanatarajiwa kujadili masuala ya mabadiliko ya tabianchi, uchumi, uvumbuzi, na maendeleo endelevu.
Antigua and Barbuda inaandaa mkutano huo, wakati huo huo ikiadhimisha miaka 45 tangu ilipopata uhuru na kujiunga na Jumuiya ya Madola mwaka 1981.