Kampuni ya Jubilee yamteua Juan Cazcarra kuwa Afisa mkuu mtendaji

Juan alijiunga na Jubilee Group Julai mwaka 2021  na kuteuliwa naibu Afisa Mkuu Mtendaji  tangu Aprili mwaka 2025.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya bima ya Jubilee imemteua Juan Cazcarra kuwa Afisa mkuu mtendaji kuanzia Disemba mosi mwaka huu.

Cazcarra anamrithi Dr Julius Kipng’etich, ambaye ameshikiwa wadhifa huo  tangu 2018, na atastaafu rasmi tarehe 30 mwezi huu.

Juan na tajriba ya zaidi ya miaka 20 katika sekta ya bima  baada ya kusimamia sekta hizo katika mabara ya Ulaya,Asia na Afrika.

Juan alijiunga na Jubilee Group Julai mwaka 2021  na kuteuliwa naibu Afisa Mkuu Mtendaji  tangu Aprili mwaka 2025.

Share This Article