Kenya na Canada zimesaini makubalulino na shirika la TBB nchini Canada utakaowezesha kubuniwa kwa mazingira bora na salama ya Wakenya kufanya kazi nchini Canada.
Mwafaka huo ulisainiwa Jumapili ukiongozwa na katibu wa Wizara ya Leba Shadrack Mwadime,Balozi wa Canada nchini Kenya Joshua Tabah na Afisa Mkuu mtendaji wa TBB Canada Lara Dyer.
Makubaliano hayo yanalenga kuhakikisha na kuwezesha mazingira salama ya kufanyia kazi nchini Canada na ushirikishwaji wa karibu wa serikali za Kenya na Canada ili kulinda haki za wafanyakazi.
Haya yanafuatia ziara iliyofanywa na ujumbe wa Kenya nchini Canada mwaka jana ukiongozwa na Katibu Mwadime akiandamana na Katibu wa uhamiaji wa wafanyakazi Joel Mwanzia.
Baadaye ujumbe wa Canada ulizuru Kenya Novemba mwaka jana kukamilisha makubaliano hayo.