Timu ya soka ya wanawake ya Kenya chini ya umri wa miaka 17 -Junior Harambee Starlets, imewasili nyumbani mapema Jumamosi kutoka Morocco, ilikoshirki fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya pili.
Starlets wanaofunzwa na Mildred Cheche waliandikisha historia walipofuzu kwa raundi ya 16 ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka huu wakishiriki kwa mara ya pili baada ya kufuzu kwa mara ya kwanza mwaka 2024.
Kenya ilimaliza ya tatu kundini E baada ya kupigwa na Uchina na Marekani,kabla ya kuititiga Samoa 4-0, katika pambano la mwisho na kufuzu kwa raundi ya 16 bora.
Hata hivyo Kenya walizidiwa maarifa walipobanduliwa na Japan mabao 3-1 .