Gor Mahia wadumisha rekodi ya asilimia 100 baada ya kuwalaza Bandari

Gor wanashikilia kukutua uongozi wa ligi hiyo kwa pointi 9 ,alama 4 zaidi ya Mara Sugar wanaokalia nafasai ya pili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Kenya,Gor Mahia wamedumisha rekodi ya asilimia 100,  baada ya kuwalemea Bandari FC bao moja kwa bila na kusajili ushindi wa tatu mtawalia msimu huu.

Mechi hiyo iliyosakatwa katika uchanjaa wa Nyayo siku ya Jumamosi ilishuhudia the Green Army, wakipata bao pekee na la ushindi kunako dakika ya 69 ya mchezo kupitia kwa Alpha Onyango.

Gor wanashikilia kukutua uongozi wa ligi hiyo kwa pointi 9 ,alama 4 zaidi ya Mara Sugar wanaokalia nafasai ya pili.

Mara Sugar walitoka sare kappa na Ulinzi Stars katika mechi nyingine ya Jumamosi katika uwanja wa Sportpesa kaunti ya Murang’a.

 

Share This Article