Maafisa nchini Ufaransa, imedhibitisha ugonjwa wa kwanza wa virusi vya Shamonda kwa binadamu.
Kulingana na mamlaka nchini humo, mgonjwa aliyeaga dunia katika hospitali moja jijini Lyon mapema mwezi Oktoba, alikuwa ameambukizwa virusi vya Shamonda.
Kwenye taarifa siku ya Alhamisi, wizara ya kilimo ya Ufaransa, iliondolea mbali hofu za kiafya zinazoweza kutambuliwa kwa umma kwa sasa.
Shamonda ni virusi vinavyoenezwa na wadudu kwa wanyama, hasa ng’ombe.
Virusi hivo viligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Nigeria katika miaka ya sitini, lakini tangu wakati huo imeripotiwa mara kwa mara katika maeneo mbalimbali barani Afrika Mashariki na Kusini, pamoja na nchini Japani.
Kufikia sasa, virusi hivyo vilichukuliwa kuwa haviwezi kuambukizwa binadamu, jambo linalomfanya mgonjwa huyo nchini Ufaransa kuwa binadamu wa kwanza kuthibitishwa kuambukizwa.
Taarifa kutoka Ufaransa ilieleza kuwa dhana kuu ni kwamba mgonjwa huyo aliambukizwa mashariki mwa Ufaransa, eneo ambalo virusi hivyo vilisambaa miongoni mwa wanyama katika majira ya ya joto mwaka huu.