FIFA World Cup:Kenya kujaribu kuepuka kufungwa magoli mengi na Marekani leo

Marekani iliwatitiga Samoa mabao 17-0 katika mchuano wa ufunguzi nao Kenya wakalimwa magoli matatu bila jawabu na Uchina .

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya wanawake walio chini ya umri wa miaka 17-Junior Harambee Starlets, itarejea katika uwanja wa Mohammed 6 leo usiku kwa mechi ya pili ya kundi E, kuwania Kombe la Dunia dhidi ya Marekani kuanzia saa tatu usiku.

Starlets wataingia mechi hiyo kwa lengo moja tu kuepuka kichapo cha fedheha ambacho huenda kiyumbishe juhudi za kufuzu kwa raundi ya mwondoano kwa mara ya kwanza.

Marekani iliwatitiga Samoa mabao 17-0 katika mchuano wa ufunguzi nao Kenya wakalimwa magoli matatu bila jawabu na Uchina .

Kenya wanaonolewa na mildred Cheche wana fursa ya kufuzu kwa mwondoano kwa mara ya kwanza endapo watazuia kufungwa magoli mengi na Marekani,na ikiwa watapata ushindi mkubwa dhidi ya Samoa siku ya Jumapili katika mechi ya mwisho.

Share This Article