Polisi wamekabiliana na waandamanaji kuanzia Jumamosi usiku hadi Jumapili huku raia kote nchini humo wakiandamana katika miji mbalimbali kulalamikia hali ngumu ya maisha.
Mioto ,uvunjaji maduka na uporaji mali vilishuhudiwa wakati maelfu ya watu waliingia barabarani kupinga kupanda kwa gharama ya maisha ,kudorora kwa viwango vya masomo katika shule za umma na huduma duni za umma.
Kulikuwa na makabiliano makali wakati polisi walirusha vitoza machozi kuwatawanya waandamanaji.
Maandamano hayo yanafuatia maandamano ya wiki nzima ya wanafunzi huku taifa hilo likisalia na miezi sita pekee kuandaa uchaguzi mkuu kumtafuta mrithi wa Rais Emmanuel Macron.
Zaidi ya waandamanaji nusu milioni walijitokeza barabarani katika maandamano hayo yaliyosababisha uharibifu mkubwa wa mali ikiwemo kuteketezwa kwa magari na maduka kadhaa.