Wakenya watawala mbio za nusu marathoni nchini Japan

Alexander Mutiso aliwaongoza Wakenya kunyakua nafasi nne bora katika mbio za wanaume

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanariadha wa  Kenya  Agnes Jebet Ng’etich na Alexander Mutiso,walitawala  mbio za nusu marathoni za Tokyo Legacy Half Marathon 2026  mapema Jumapili.

Jebet Ngetich aliyeshinda ubingwa wa dunia katika mbio za barabarani mwezi jana nchini Denmark,aliweka rekodi mpya ya dunia ya shindano hilo akikata utepe kwa saa 1 dakika 4 na sekunde  23.

Tabitha Njeri pia wa Kenya alitwaa nafasi ya pili kwa saa 1 dakika 8 na sekunde 28, huku Kazuna Kanemoto wa Japan akihitmisha nafasi tatu bora.

Alexander Mutiso aliwaongoza Wakenya kunyakua nafasi nne bora katika mbio za wanaume kwa muda wa  dakika 59 na sekunde 51,akifuatwa na Sitonik Kiprono na James Mutuku katika nafasi za pili na tatu mtawalia.

 

Share This Article