Tusker FC kuikabili Singida Black Stars uwanjani Nyayo

Dismas Otuke
1 Min Read

Tusker FC watakuwa na kibarua kigumu Jumapili alasiri watakapowaalika Singida Black Stars  kutoka Tanzania, katika mkumbo wa kwanza mchujo wa pili kuwania kombe la Shirikisho barani Afrika.

Wanabururi  Tusker, walifuzu kwa mchujo wa pili kufuatia ushindi wa jumla wa mabao 3-2, dhidi ya Madani ya Sudan Kusini, katika mchujo wa kwanza, wakati Singida wakiiparamia Al Ghazala ya Sudan Kusini magoli 10-1.

Mkumbo wa pili utachezwa nchini Tanzania wiki ijayo huku mshindi wa jumla akifuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Share This Article