Somalia kuandaa uchaguzi mkuu Mei 15 mwaka ujao

Somalia hata hivyo inakabiliwa na changamoto ya kiusalama kutokana na vita vya mara kwa mara vinanvyoongozwa na kundi haramu la Al Shaabab.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya uchaguzi nchini Somalia imetangaza kuwa uchaguzi mkuu utaandaliwa Mei 15 mwaka ujao baada ya kuahirishwa kwa mwaka mmoja.

Muhula wa kuhudumu kwa Rais Hassan Sheikh Mohamud ulikamilika Mei mwaka huu lakini bunge likapiga kura kuongeza mwaka mmoja ,hatua iliyopingwa vikali na wabunge wa upinzani.

Rais Mohamud amekuwa akijaribu kueleta mfumo wa uchaguzi wa kidemokrasia nchini Somalia ili kuondoa mfumo wa sasa ambapo viongozi wa kimbari humchagua kiongozi,lakini amekabiliwa na shutuma na upinzani mkali.

Kulingana na tume ya uchaguzi ,uchaguzi wa ubunge utaandaliwa Aprili 15, ukifuatwa na ule wa Urais mwezi mmoja baadaye.

Somalia hata hivyo inakabiliwa na changamoto ya kiusalama kutokana na vita vya mara kwa mara vinanvyoongozwa na kundi haramu la Al Shaabab.

Share This Article