Uchunguzi wa hivi punde kuhusiana na sakata ya Kombe la Dunia nchini Ghana umebaini kuwa zaidi ya watu 30 walisafiri kuhudhuria fainali hizo za mwezi Juni na Julai wakisingizia kuwa maafisa wa mamlaka ya Utalii nchini humo(GTA).
Takwimu kutoka ubalozi wa Marekani nchini Ghana zimeonyesha kuwa licha ya bodi ya Utalii kuwa na maafisa 11 pekee orodha ya watu 30 waliodaiwa kuwa wanafanyakazi wa GTA walituma maombi ya Viza katika ubalozi wa Marekani.
Mbunge wa upinzani Vincent Ekow Assafuah anadai kuwa orodha ya 50, waliojumuishwa katika orodha kama Wanahabari ni wawili pekee ambao ni wanahabari halisi.
GTA ilitumia dola 14,000 za Marekani saa na shilingi milioni 1.8 za Kenya kwa kutuma maombi ya viza kwa watu hao waliokuwa wasafiri kwenda Marekani.
GTA hata hivyo imekanusha madai hayo huku uchunguzi ukianzishwa.